Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, mifumo ya mahakama duniani haiwezi kubadilishwa kupitia teknolojia, utungaji wa sheria au mageuzi ya kitaasisi pekee. Mustakabali wa mabadiliko hayo unategemea watu wenye uelewa wa kina wa sheria, wanaofanya juhudi za kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo yana maana na kuleta matokeo yanayokusudiwa.
Kwa mawakili tisa vijana wa kike wa Palestina, suala hili limepata umuhimu mpya. Baada ya miezi kumi ya kujifunza, kupata mwongozo wa kitaaluma na kushiriki katika shughuli za vitendo, wamefanikiwa kuhitimu kundi la kwanza la programu za mafunzo za Kituo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Birzeit, kinachojulikana kama Hüqooq-Tech Legal Incubator.
Mafanikio yao ni zaidi ya kukamilisha kozi ya kuendeleza taaluma, yanaonesha jinsi uwekezaji katika kizazi kijacho cha wataalamu wa sheria unavyoweza kuziba pengo kati ya elimu ya kitaaluma inayotolewa vyuoni na utekelezaji wa sheria katika mazingira halisi. Hatua hii inalenga kuleta athari katika mustakabali wa Palestina, kufungua njia mpya za ajira na kuimarisha msingi wa rasilimali watu kwa ajili ya mageuzi ya mfumo wa mahakama.
Sour Qasimi, mmoja wa wanawake walioshiriki katika mafunzo hayo, alisema: “Ushahidi wa kidijitali, mashtaka ya kisheria, haki za kidijitali na mikataba ya kielektroniki vilikuwa maeneo mapya kwangu. Leo, nina ujasiri wa kutosha wa kueleza masuala haya, kuyajadili na kuwasaidia wengine kuyaelewa kupitia kesi halisi na mifano ya vitendo.”
Chanzo: Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Maoni yako